Jobs & Careers

Mathematics/Chemistry or Mathematics/Physics Teaching Jobs at Our Lady Of Angels Academy

Mathematics/Chemistry or Mathematics/Physics Teaching Jobs at Our Lady Of Angels Academy

Mathematics/Chemistry or Mathematics/Physics Teaching Jobs at Our Lady Of Angels Academy

History/Kiswahili or Kiswahili/CRE Teaching Jobs at Our Lady Of Angels Academy
Mathematics/Chemistry or Mathematics/Physics Teaching Jobs at Our Lady Of Angels Academy

EDCI 337: MBINU ZA KUFUNDISHA KISWAHILI-MBINU ZA UFUNDISHAJI

A. MAJADILIANO
– Kulingana an wanjala na wengine (2003) majadiliano ni mazungumzo baina ya watu kuhusu jambo fulani
– Kamusi ya TUKI (2003) Ni mazungumzo ya watu wawili au Zaidi wanaobadilishana mawazo kuhusu mada Fulani.

SIFA ZAKE.
1. Uhusisha watu Zaidi ya mmoja
2. Mbinu hii yaweza kutumika na mbinu zingine za kufundisha
3. Uhusisha ushirikishi hai baina ya mwalimu Na mwanafunzi.

Matayarisho
1. Kuteua mada
2. Kuandaa majadiliano
– madadiliano ghafla- mwalimu kuandika mada na kuwapa wanafunzi kujadili hapo kwa hapo
– Majadiliano hadhara –mwalimu huandika mada mbalimbali na wanafunzi huwa na wakati wa kutafitia

Mambo muhimu ya kuzingatia
1. Mahali pa majadiliano pawe patulivu pasipo na usumbufu
2. Mwalimu hasitawale majadiliano
3. Mwanafunzi anapowasilisha lazima wenzake wanyamaze wasikilize
4. Kila mwanafunzi hashiriki katika majadiliano
5. Majadiliano yatumie muda mwafaka
6. Idadi ya wanafunzi iwe ya wastani.
7. Mwalimu atoe madhumuni ya majadiliano

UMUHIMU WA MAJADILIANO
1. Humsaidia mwanafunzi kuwa na ujasiri wa kuzungumza hadharini.
2. Huchangia kukuza stadi kusikiliza na kuzungumza
3. Hukuza lugha na sarufi ya mwanfunzi kwa jumla
4. Hukuza matamshi bora miongoni mwa wanafunzi
5. Mwanafunzi hupanua msamiati wao wanapojadiliana
6. Huwa ni mizani ya kupima wanafunzi katika stadi za kuzungumza na kusikiliza
7. Wanafunzi hupanua fikra zao kuhusu maswali wanayojadiliana
8. Huwasaidia wanafunzi kujifunza na kufikiria.

UDHAIFU
a. Wanafunzi wenye ujasiri hutawala majadiliano
b. Huitaji muda mwingi
c. Kuna uwezekano wa mwalimu kushindwa kudhibiti darasa
d. Mchemko wa hasira kwa baadhi ya wanafunzi huadhiri mawasiliano darasani.
e. Huenda wanafunzi wenye ukwasi wa lugha wakawa ndio wanazungumza
f. Muda kupotea ikiwa wanafunzi wanapotoka kidogo
g. Wanfunzi wengine hutoka nje ya mada.

B. MBINU YA MAKUNDI
Uhusisha wanafunzi hai ili kuwafutia suluhu jambo fulani. Ni mbinu shirikishi ambayo mwalimu anawagawa wanfunzi katika amkundi mbalimbali.

SIFA ZA MAKUNDI
1. Hushirikisha kila mwanafunzi
2. Hufikirisha mwanafunzi
3. Humwondolea mwanafunzi woga au unyonge.
4. Mwanafunzi huwa mbunifu
5. Huchochea udadisi

MATAYARISHO
– Mwalimu abainishe shabaha ambazo analenga kufikia baada ya kazi ya makundi.
– Mwalimu atathmni iwapo shabaha hizo zitaafikiwa katika mbinu ile ya amkundi
– Changua swala ambalo litawausisha wanafunzi sana bila mwalimu kujihusisha.
– Mwalimu awasawazishe wanafunzi wote.
– Changua swala rahisi kwanza
– Tayaarisha malighafi yanayofaa

UMUNIMU WA MAKUNDI
1. Huchochea uhusiano bora baina ya mwalimu na mwanafunzi na pia wanafunzi na wanafunzi wenzake
2. Kila mmoja hupata nafasi ya kutoa maoni/mawazo yake
3. Hujenga hali ya mashindano.
4. Hukuza uwezo wa kuwaza na kukumbuka

UDHAIFU
1. Hutumia muda mrefu
2. Mambo machahe hufundishwa na uwezekano wa kumaliza mada ni mdogo.
3. Huweza kujenga huasama kati ya wanafunzi-wenye uwezo mkubwa na mdogo.
4. Wamnafunzi wenye uwezo wa chini kutolipenda somo lile.
5. Mahusiano mabaya kati ya wanafunzi ikwa mwalimu hata simamia kati ya mambo wanayojadili.

C. MAONYESHO.
Inahusu utazamaji wa picha .filamu n.k

Vipengee vya kuzingatia
– Wakati/muda

 

– Mada na malengo
– Uwepo wa rasilimali
– Hali ya maumbile ya mwanafunzi

Umuhimu
1. Hukuza uwezo wa kukumbuka
2. Huokoa wakati- kueleza kwa haraka
3. Huchangamsha mwanafunzi
4. Uimarisha ubunifu wa mwalimu
5. Huwasaidia wanafunzi kutangamana.
6. Mada hueleweka kwa urahisi

Udhaifu
1. Mwalimu hushindwa kuwatathmni wanafunzi
2. Huitaji muda mwingi kutengemea aina ya maonyesho
3. Haizingatii hali tofauti za maumbile za wanafunzi k.v walio na shida za macho
4. Mada nyingine ni ngumu kutumia maonyesho k.v kiimbo na shada katika sarufi na matumizi ya lugha.

D. HADITHI
Ni utungo wenye visa vya kubuni na huwasilishwa kwa lugha ya kinadhari kwa kusudi la kuburudisha, kukuza maadili na kuunganisha jamii.

Sifa za hadithi
1. Ina mianzo maalum
2. Mwisho maalum
3. Funzo fulani
4. Masimulizi yake ni ya wakati uliopita
5. Lugha ya kinadhari
6. Wahusika wanyama na binadamu

Matayarisho ya mwalimu
– Hatumie mifano halisi
– Hatunge hadithi iliyo na kisha fulani atakachotumia katika ualishaji wake.

Umuhimu wa hadithi kama mbinu ya ufundishaji
– Hukuza uwezo wa mwanafunzi wa kusikiliza na kuelewa
– Hukuza ubunifu wa wanafunzi
– Kuimarisha lugha mfano msamiati
– Kuvuta makini ya wanafunzi
– Kuburudisha wanafunzi

Udhaifu
– Ukosefu wa vifaa
– Ukosefu wa ubunifu wa mtambaji.
– Huitaji mada nyingi
– Si rahisi kutumia mifano hai kwaivyoyaitaji mtambaji kutumia teknolojia ambayo huenda isipatikane. MHADHARA

Mbinu hii imekashifiwa.

Mhadhara rasmi– mwalimu uhusisha wanafunzi katika kipindi
Mhadhara usiorasmi– uhusisha mwalimu kufunza kisha kuwapa wanafunzi nafasi ya kuuliza maswali. Wanafunzi uhusishwa darasani. Kuna majibu ya moja kwa moja. Huitaji mwalimu kuwa na ufahamu wa somo kabla ya kipindi.

Matayarisho
– Kutumia chati kabla ya kipindi
– Kutmia lugha ya mwili

Umuhimu
– Huokoa muda
– Kufundisha wanafunzi wengi kwa wakati mmoja
– Ni njia bora ya kufundisha ufahamu wa kusikiliza
– Guzidisha umakinifu
– Mwalimu huweza kutathmini wanafunzi kupitia maswali na majibu
– Hutumika pamoja na mbinu zingine ili kuafikia shabaha zake.

Udhaifu
– Hujenga hali ya woga na kutojiamini kwa wanafunzi
– Haileti ukombozi wa fikra.
– Haishirikishi wanafunzi kikamilifu.
– Vielelezo vichache

E. UIGIZAJI
– Mavazi maalum huweza kuvaliwa yaani maleba.
– Matendo na sauti za watu huweza kuigwa na pia hata sauti za wanyama ili kupitisha ujumbe.
– Hadhira huwa katika makundi wakati wa uigizaji ili kupata mfulululizo wa matendo na pia mtiririko.
– Hushirikisha hadhira aidha kwa wimbo au kutenda matendo fulani

Aina
1. Uigizaji jukwaani
2. Uigizaji uhusishi

Sifa
1. Hushirikisha hadhira na waigizaji
2. Uhusisha matumizi ya mavazi maalum
3. Huweza kuandamana na vyombo maalum
4. Huwa na madhari au pahala maalum matendo yanapofanyika.
5. Huweza kuandamana na miondoko ya mwili.
6. Uhusisha adhira hai.
7. Uambatanisha vifaa vya ufundishaji.

Umuhimu.
a. Hukuza vipawa au talanda za wanafunzi.
b. Huwasilisha hoja kwa njia nyepesi.
c. Huondoa uchovu.
d. Mwanafunzi huwa na hupana w kufikiria
e. Hufanya ufundishaji kuwa hai kwani vitendo ni moja kwa moja. Huleta utangamano wa wanafunzi.

Udhaifu
1. Muda mwingi
2. Baadhi ya vyombo huwa za bei ghali
3. Matendo yaweza kuchukuliwa kwa mzaha hivyo kukosa maana.
4. Hii mbinu haiwezi jisimamia.
5. Haihusishi wanafunzi wote
6. Uitaji ubunifu wa mwalimu.

F. UFUNDISHAJI KIKOA
– Ni ufundishaji wa pamoja unaojumulisha waalimu wawili au Zaidi kutumia wanafunzi wa kiwango kimoja.
– Waalimu hukutana na kujadili kabla ili kutoa nyenzo mbalimbali watakaotumia katika ufundishaji.

ZIARA NYANJANI
Sifa
o Huwa na lengo mahususi
o Mpangilio na utaratibu maalum
o Uhusisha upelelezi na ugenduzi wa mambo mapya

Matayarisho
– Wanafunzi huitaji kupewa maswali kuhusu wanachoshungulikia
– Hulenge shabaha ya matayarisho.
– Hatua zifuatwe moja kwa moja.
– Tambua idadi ya wanafunzi.
– Wanafunzi watahadharishwe kuhusu eneo watakaozuru.
– Sharia na taratibu za eneo hilo zijulikane kwa wanafunzi na kufuatwa

Umuhimu
– Huongeza kuelewa kwa wanafunzi
– Kuimarisha uwezo wao wa kukumbuka.
– Huondoa uchovu na uchoshi.
– Huleta utangamano.
– Hufanya mafunzo kuwa rahisi.

Udhaifu
– Muda mwingi
– Huitaji fedha- gharama
– Mwalimu anahitaji kuwa mbunifu ili aunde hatua watakaofuata.

Hatua
Kabla ya ziara
– Mwalimu hawe ameteua mada na awe na shabaha tayari.
– Idhi kutoka kwa mkuu wa shule, wazazi ,eneo hilo
– Vifaa vitakavyo hitajika.
– Mwalimu awaelekeze wanafunzi ipasavyo.

Wakati wa ziara
-Wazingatie lugha sanifu

Baada ya ziada.
-Wanafunzi wajadiliane matokeo ya ziara.
-Ripoti iandikwe kwa usaidizi wa mwalimu.

G. MASWALI NA MAJIBU
Jinsi ya kuitumia
o Kutathmini yaliyo funzwa wakati uliotangulia na baadaye
o Muhtasari wa kipindi.
o Kuwahusisha wanafunzi ili waweze kuchangia na kushiriki kikamilifu
katika somo na kuamsha ari ya kufikiria Zaidi.

UMUHIMU
o Mwalimu hutoboa kama ameafiki shabaha.
o Udhaifu wa wanafuzi

UDHAIFU
o Mwalimu asipouliza maswali yake vyema hataweza kuwajua wanafunzi.
o Mwalimu hulenga wanafunzi kadhaa darasani
o Muda
o Tofauti za uelewaji wa wanafunzi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button